Hamia kwenye habari

Mwonekano wa jinsi jengo lenye orofa nne nchini Angola utakavyokuwa baada ya ukarabati kukamilika

APRILI 25, 2022
ANGOLA

Jengo Lililofanyiwa Ukarabati Litatumiwa Katika Upanuzi wa Ofisi ya Tawi ya Angola

Jengo Lililofanyiwa Ukarabati Litatumiwa Katika Upanuzi wa Ofisi ya Tawi ya Angola

Ukarabati umeratibiwa kuanza Juni 2022 katika jengo lenye orofa nne ambalo litaandaa maeneo ya ziada ya makao na ofisi kwa ajili ya ofisi ya tawi ya Angola. Kwa sasa, hakuna nafasi ya kutosha kwa ajili ya washiriki 207 wa familia ya Betheli katika ofisi ya sasa, ambayo ilijengwa mwaka wa 2003.

Nafasi hiyo ya ziada inahitajika kwa sababu baadhi ya washiriki wa familia ya Betheli wanaishi katika majengo yaliyokodiwa. Akina ndugu walinunua jengo hilo Desemba 2021. Jengo hilo liko umbali mfupi kutoka kwenye ofisi ya tawi ya sasa.

Jengo hilo linalofanyiwa ukarabati litakuwa na vyumba 57 na ofisi 60. Vyumba hivyo vitakuwa na ofisi chumbani, na maeneo ya ofisini yatakuwa na maeneo ya wazi na ofisi zilizofungwa. Jengo hilo jipya litakuwa pia na chumba cha kufanyia mikutano na cha matumizi mbalimbali. Eneo la ofisi litakuwa na kuta zinazoweza kuondolewa, kurudishwa, na kuhamishwa ili kukidhi mahitaji yanayobadilika.

Washiriki wa familia ya Betheli ambao kwa sasa wanaishi katika nyumba za kupanga wanatarajiwa kuhamia katika jengo hilo mnamo Februari 2024.

Samuel Campos, mshiriki wa Halmashauri ya Tawi ya Angola anasema hivi: “Tumekuwa tukisali na kufanya kazi pamoja na Idara ya Ulimwenguni Pote ya Usanifu Majengo na Ujenzi ili kushughulikia uhitaji wa nafasi zaidi. Ununuzi na ukarabati wa jengo hili ni jibu la Yehova kwa sala zetu.”

Kuna zaidi ya wahubiri 160,000 nchini Angola. Zaidi ya watu 400,000 walihudhuria Ukumbusho mwaka uliopita, na wahubiri waliongoza zaidi ya mafunzo 200,000 ya Biblia. Tuna uhakika kwamba Yehova atabariki kazi ya ukarabati wa jengo hilo jipya la ofisi ya tawi ambalo litasaidia kuendeleza masilahi ya Ufalme.​—1 Mambo ya Nyakati 29:16.