Hamia kwenye habari

Juu: Ndugu Yevgeniy Bochko, Ndugu Vladimir Kolesnikov, na Ndugu Aleksey Shubnikov

Chini: Ndugu Vitaliy Ushakov na Ndugu Valeriy Vechkayev

FEBRUARI 13, 2024
URUSI

Wanakazia Fikira Heshima ya Kumtumikia Yehova

Wanakazia Fikira Heshima ya Kumtumikia Yehova

Mahakama ya Wilaya ya Vyselkovskiy iliyo katika Eneo la Krasnodar itatangaza uamuzi wake hivi karibuni katika kesi inayowahusu Ndugu Yevgeniy Bochko, Ndugu Vladimir Kolesnikov, Ndugu Aleksey Shubnikov, Ndugu Vitaliy Ushakov, na Ndugu Valeriy Vechkayev. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tuna uhakika kwamba Yehova ataendelea kuwapa nguvu na shangwe ndugu hao na wale wote wanaoendelea kumtegemea ili kupata msaada.​—Zaburi 141:8.

Mfuatano wa Matukio

  1. Februari 11, 2022

    Kesi ya uhalifu ilifunguliwa dhidi ya Yevgeniy, Aleksey, Vitaliy, na Valeriy

  2. Februari 13, 2022

    Nyumba zilifanyiwa msako. Yevgeniy, Aleksey, na Vitaliy walihojiwa. Vitaliy aliwekwa kizuizini

  3. Februari 15, 2022

    Vitaliy alipelekwa mahabusu

  4. Februari 16, 2022

    Yevgeniy na Aleksey waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Februari 18, 2022

    Valeriy aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Februari 21, 2022

    Kesi ya uhalifu ilianzishwa dhidi ya Vladimir

  7. Machi 15, 2022

    Vladimir aliwekewa vizuizi vya kusafiri. Kesi za uhalifu ziliunganishwa na kuwa kesi moja

  8. Septemba 8, 2022

    Vitaliy aliachiliwa kutoka mahabusu na kuwekwa katika kifungo cha nyumbani

  9. Oktoba 10, 2022

    Vitaliy aliachiliwa kutoka katika kifungo cha nyumbani na kuwekewa vizuizi vya kusafiri

  10. Mei 31, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza