Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 114

“Iweni na Subira”

“Iweni na Subira”

(Yakobo 5:8)

  1. 1. Yehova, Baba yetu,

    Anapenda jina lake.

    Ataka litakaswe,

    Lawama liondolewe.

    Kavumilia mengi,

    Tena muda mrefu;

    Ana subira nyingi,

    Hajachoka kamwe.

    Ataka watu wote

    Wapate kuokolewa.

    Aonyesha subira,

    Kwa faida yetu sote.

  2. 2. Nasi tunahitaji,

    Kuionyesha subira.

    Ghadhabu tuepuke.

    Tukae kwa utulivu.

    Tuzingatie mema,

    Wafanyayo wengine.

    Tutumaini mema,

    Japo matatizo.

    Na sifa za Kikristo,

    Tuonyeshe sikuzote.

    Na kwa kufanya hivyo,

    Tumuige Mungu wetu.