Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 132

Sasa Tumekuwa Mwili Mmoja

Sasa Tumekuwa Mwili Mmoja

(Mwanzo 2:23, 24)

  1. 1. Huyu ndiye, mfupa wangu

    Mwili wangu, nina mwenzangu.

    Mungu amenipa mwenzi,

    Ninayempenda.

    Tumekuwa mwili mmoja,

    Tupate baraka za Mungu.

    Mume na mke pamoja,

    Familia moja.

    Daima tumtumikie.

    Atuongoze,

    Tupendane kikweli.

    Tuapavyo, iwe hivyo

    Tupate shangwe na furaha.

    Tumheshimu Yehova,

    Sikuzote uwe wangu.