Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 151

Atawaita

Atawaita

(Ayubu 14:13-15)

  1. 1. Lo! Uhai ni kama ukungu,

    Leo, kesho haupo.

    Watokea kisha watoweka.

    Huzuni kwa wapendwa.

    Mtu akifa, je, ataishi?

    Mungu ameahidi:

    (KORASI)

    Yehova atawaita

    Watoke na kuishi.

    Kwani anatamani,

    Kazi ya mikonoye.

    Usiwe na shaka kamwe,

    Mungu atamwinua,

    Kisha twishi milele,

    Tu mali yake yeye.

  2. 2. Rafikize Yehova wakifa,

    Hawasahau kamwe.

    Walalao katika Kaburi,

    Watainuka tena.

    Tufurahie uzima nao,

    Duniani milele.

    (KORASI)

    Yehova atawaita

    Watoke na kuishi.

    Kwani anatamani,

    Kazi ya mikonoye.

    Usiwe na shaka kamwe,

    Mungu atamwinua,

    Kisha twishi milele,

    Tu mali yake yeye.