Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 29

Kuishi Kulingana na Jina Letu

Kuishi Kulingana na Jina Letu

(Isaya 43:10-12)

  1. 1. Yah Mweza Yote, Mungu wa milele,

    U mwenye haki, upendo, nguvu.

    Chanzo cha kweli na hekima yote,

    Mtawala Mwenye Enzi Kuu.

    Twafurahia kukutumikia,

    Kweli ya Ufalme twatangaza!

    (KORASI)

    Ni pendeleo kuwa Mashahidi.

    Ee, na tuishi kwa jina letu!

  2. 2. Tufanyapo kazi, bega kwa bega,

    Upendo unatuunganisha,

    Kufunza kweli na kukutukuza;

    Hutupa sisi furaha tele.

    Twaitwa kwa jina lako Yehova;

    Twapendelewa kukupa sifa!

    (KORASI)

    Ni pendeleo kuwa Mashahidi.

    Ee, na tuishi kwa jina letu!