Hamia kwenye habari

Sera ya Ulimwenguni Pote ya Kutumia Taarifa za Kibinafsi

Sera ya Ulimwenguni Pote ya Kutumia Taarifa za Kibinafsi

Tunakusanya, kuhifadhi, na kutumia taarifa zako za kibinafsi ili tu kutimiza kusudi au makusudi ambayo yalikufanya uzitoe na zinaendelea kuwa katika kumbukumbu zetu kwa muda ambao zinahitajika ili kutimiza kusudi hilo au ikiwa kuna sababu nyinginezo za kisheria. Kwa hiyo ikiwa utaamua kwamba hutatupatia taarifa zozote za kibinafsi tunazokuomba, itakuwa vigumu kwako kufungua baadhi ya sehemu katika tovuti yetu au kutumia programu nyingine za Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc. pia, itakuwa vigumu kwetu kujibu ombi lako.

Taarifa tunazopata kupita maombi mbalimbali zinawafikia wale wanaohusika katika kutimizwa kwa kusudi la ombi lako na wataalamu wanaoshughulikia kiufundi utendaji na udumishaji wa tovuti na programu zinazohusiana. Hatutoi taarifa zako za kibinafsi kwa mtu mwingine isipokuwa (1) tunapohitaji kufanya hivyo ili kuandaa huduma ambayo uliomba na tumekupa taarifa kamili, (2) tumeona kwamba tunalazimika kutoa taarifa hizo ili kutii sheria zilizowekwa, (3) wenye mamlaka wanapoziomba, au (4) taarifa hizo zinapohitajika kwa sababu za kiusalama, kwa sababu za kiufundi, au ili kuzuia ulaghai. Unapotumia tovuti hii na programu nyingine zinazohusiana na hii, unaturuhusu kutoa taarifa zako kwa mtu wa tatu kwa ajili tu ya makusudi tuliyozungumzia. Taarifa zozote za kibinafsi unazotoa hazitauzwa au kukodishwa kwa sababu yoyote ile.

MATUMIZI YA TAARIFA ZA KIBINAFSI KWENYE TOVUTI

Sehemu nyingi za tovuti hii hazihitaji ujisajili wala kutuma taarifa zozote kwetu ili uzitumie. Hata hivyo, baadhi ya sehemu zinaweza kutumiwa na watumiaji waliojisajili tu, wale waliotuma maombi, au wale ambao taarifa zao za kibinafsi zimetumwa kwetu kutoka katika kutaniko la Mashahidi wa Yehova kupitia jw.org. Tutashughulikia taarifa zako za kibinafsi kulingana na vile ulivyokubali zitumiwe. Katika visa vingine, hata kama umevunja makubaliano, tunaweza kuwa na msingi halali wa kisheria wa kuendelea kushughulikia taarifa zako, ikiwa matakwa ya kisheria yanaturuhusu kufanya hivyo.

Taarifa za kibinafsi tunazopata kutoka kwako zilizoko kwenye tovuti yetu zinatumiwa kwa makusudi uliyoelezwa ulipojaza maombi. Makusudi hayo yanaweza kutia ndani mambo yafuatayo:

Akaunti. Anwani ya barua-pepe unayotumia unapofungua akaunti katika tovuti hii itatumiwa kuwasiliana nawe kuhusiana na akaunti yako. Kwa mfano, ukisahau jina lako la mtumiaji au nywila (neno la siri) yako na kuomba usaidiwe kuingia kwenye tovuti, utasaidiwa kupitia ujumbe utakaotumwa kwenye anwani ya barua-pepe uliyojaza kwenye wasifu wa mtumiaji.

Maombi. Ikiwa unastahili kulingana na mafundisho na sera za Mashahidi wa Yehova, unaweza kutumia tovuti hii kufungua akaunti ya kibinafsi, kutuma maombi, au kutaniko lako linaweza kutumia tovuti hii kutuma maombi kwa niaba yako ikiwa ungependa kuongeza utumishi wako wa kidini. Taarifa zako za kibinafsi zilizo katika maombi yako zinaweza kutia ndani taarifa za kibinafsi ulizoandika, zilizoandikwa na wazee wa kutaniko lako, au mwangalizi wa mzunguko. Katika kisa kama hicho, taarifa hizo zitatumika tu kwa ajili ya kushughulikia na kuzingatia maombi yako na kwa madhumuni ya usimamizi, kutia ndani kuingiza maelezo yanayokuhusu yakiwa sehemu ya mchakato wa kushughulikia ombi. Ikihitajika, ili kushughulikia maombi yako taarifa zako zinaweza kupelekwa katika ofisi nyingine za tawi, makao makuu ya Mashahidi wa Yehova, au mashirika mengine yanayotumiwa na Mashahidi wa Yehova katika nchi mbalimbali. Katika visa vyote, kila ombi linashughulikiwa peke yake, hakuna maombi yanayoshughulikiwa kielektroni.

Ukurasa wa Maelezo Yangu: Baada ya kufungua akaunti, huenda mwandishi wa kutaniko lako akakuwezesha kutumia sehemu ya Maelezo Yangu. Ukiamua kuongeza habari zako za kibinafsi kwenye ukurasa wa Maelezo Yangu kwenye hub.mr1310.com, utaulizwa ikiwa unakubali habari hizo za ziada zitumiwe kukutambulisha kwa ajili ya matumizi zaidi na ili kuwasiliana nawe. Ukisaidia katika mradi fulani na kuongeza habari kuhusu ustadi wako kwenye ukurasa wa Maelezo Yangu, mkaguzi wa ustadi anaweza kuchunguza ustadi wako kupatana na mradi huo. Ili taarifa zako zishughulikiwe, huenda pia, ikihitajika, zikashirikiwa na ofisi nyingine za tawi za Mashahidi wa Yehova, au na mashirika mengine yanayotumiwa na Mashahidi wa Yehova katika nchi mbalimbali.

Madarasa ya Mazoezi: Ikiwa unastahili kushiriki katika miradi, kutia ndani miradi ya ujenzi, mtu anayepanga madarasa ya mazoezi anaweza kukualika kuhudhuria darasa. Unaweza kukubali au kukataa mwaliko au ufute uhudhuriaji kabla ya kuanza kwa darasa hilo. Ukikubali mwaliko, wazoezaji wa darasa hilo wataweka rekodi ya uhudhuriaji wako, wataje ulitimiza malengo gani kwa kuhudhuria darasa hilo, na huenda wakaandika maelezo fulani. Wanaopanga madarasa na pia wazoezaji wataweza kuangalia na kuchanganua ustadi ulioongeza kwenye ukurasa wako wa Maelezo Yangu kwenye hub.mr1310.com. Ili taarifa zako zishughulikiwe, huenda zikashirikiwa na ofisi nyingine za tawi za Mashahidi wa Yehova, makao makuu ya ulimwenguni pote ya Mashahidi wa Yehova, au na mashirika mengine yanayotumiwa na Mashahidi wa Yehova katika nchi mbalimbali.

Michango. Ukitoa mchango wa pesa mtandaoni, tutahitaji jina lako na anwani au namba ya simu. Michango inayotolewa kupitia kadi za benki, hushughulikiwa na kampuni zinazotegemeka zinazotoa huduma za kuhamisha pesa mtandaoni na ambazo zina sera za ulinzi na usalama wa taarifa za kibinafsi zinazotambulika duniani pote. Tunaweza kupokea taarifa zako za kiuchumi, kama vile namba ya kadi ya benki au namba ya akaunti ya benki ili kushughulikia michango yako, na kutuma habari zinazohitajiwa na wale wanaotoa huduma. Tunashughulikia mchango wako kwa njia salama ambazo zinapatana na viwango vya usalama wa taarifa za malipo (Payment Card Industry Data Security Standard). Anayepokea mchango atahifadhi rekodi ya kupokea pesa hizo kwa angalau miaka kumi. Rekodi hiyo inatia ndani rekodi ya tarehe ambayo mchango ulitolewa, kiasi kilichotolewa, na njia iliyotumiwa. Hivyo, tutaweza kwenda sambamba na masharti ya uhasibu na kujibu maswali yoyote kutoka kwako kwa kipindi hicho. Hatutawasiliana nawe ili kuomba michango zaidi.

Maombi ya Kupata Habari Zaidi au Kujifunza Biblia. Unaweza pia kuomba habari zaidi au kujifunza Biblia kupitia tovuti yetu. Tutatumia tu taarifa za kibinafsi ulizotuma kwenye maombi yako kulingana na kile unachohitaji. Taarifa zako zinaweza kupelekwa kwenye ofisi nyingine za tawi au mashirika mengine yanayotumiwa na Mashahidi wa Yehova ikiwa ni muhimu kufanya hivyo ili kutekeleza maombi yako.

Makusudi Mengine. Unaweza kutuma taarifa zako za kibinafsi (kama vile jina, anwani ya posta, na namba ya simu) kwa ajili ya makusudi mengine tofauti na kufungua akaunti, kutuma maombi, au kutuma mchango. Katika kila kisa, kusudi la kuombwa utupatie taarifa hizo zinakuwa wazi kabisa. Hatutatumia taarifa zako unazotupatia kwa ajili ya mambo ambayo huelezwi unapozitoa.

MATUMIZI YA TAARIFA ZA KIBINAFSI KWENYE JW LIBRARY

Habari kuhusu jinsi taarifa zako za kibinafsi zinavyotumiwa na JW Library zinapatikana kwenye ukurasa wa Programu ya JW Library Inavyotumia Taarifa Zako.

Maelezo katika ukurasa huo yanaonyesha kwamba programu hiyo inapata habari zake kwa kuzipakua kutoka kwenye tovuti ya jw.org. Tovuti hiyo ina uwezo wa kutambua anwani ya kifaa cha mtumiaji anapopakua. Taarifa zinakusanywa na tovuti ili kutoa huduma katika programu ya JW Library, kuiboresha na kuidumisha ikiwa salama. Kihususa zaidi, taarifa hizo zina matumizi yafuatayo: kumwezesha mtumiaji kufungua na kutumia programu hiyo, kuendesha na kuboresha programu hiyo, kutambua na kuzuia ulaghai na programu nyingine zilizokusudiwa kuleta madhara, na kushughulikia matukio yanayotishia usalama wa programu ya JW Library.

KUTUMA TAARIFA NCHI NYINGINE

Shirika hili la kidini linafanya kazi ulimwenguni pote kupitia mashirika mbalimbali ya kisheria. Baadhi ya vifaa vinavyotoa huduma katika tovuti hii na programu zinazohusiana na tovuti hii viko Marekani. Tunaweza kutuma taarifa zako katika nchi nyingine, kutia ndani nchi ambako sheria zao za kulinda taarifa ni tofauti kabisa na sheria za kulinda taarifa za nchi unamoishi. Tunaposhughulikia na kutuma taarifa zako za kibinafsi, tunachukua hatua madhubuti kulinda taarifa zako. Tunatarajia kwamba mashirika yote yanayotumiwa na Mashahidi wa Yehova na yanayotegemeza kazi yao yafuate sera zetu za kulinda taarifa na sheria na taratibu hususa za taarifa za kibinafsi.

Kwa kutembelea tovuti hii na kuwasiliana nasi katika mtandao unaonyesha kwamba unakubali taarifa zako zitumwe kwenye nchi nyingine. Katika visa vingi, tunatumia makubaliano ili kutuma taarifa, kama vile mikataba inayohusiana na kulinda taarifa.

HAKI ZAKO

Wakati wowote unapotuma taarifa za kibinafsi, tunachukua hatua zinazofaa kuhakikisha kwamba taarifa zako za kibinafsi ni sahihi na zinarekebishwa kwa ajili ya makusudi yaleyale yaliyofanya zikusanywe. Kwa kutegemea nchi unayoishi na sheria zinazokubalika za kulinda taarifa, unaweza kuwa na haki zifuatazo kuhusiana na taarifa za kibinafsi unazotutumia:

  • Unaweza kuomba habari kuhusu jinsi taarifa hizo za kibinafsi zinavyokusanywa na kutumiwa kulingana na sheria zinazokubalika katika nchi yenu.

  • Unaweza kuomba kuingia, kufunga, kufuta, au kurekebisha taarifa zako za kibinafsi ikiwa hazijakamilika au si sahihi.

  • Ikiwa ni halali kisheria kufanya hivi, unaweza kuomba taarifa zako za kibinafsi zisiendelee kushughulikiwa.

Ikiwa nchi unayoishi ina sheria zinazokubalika za kulinda taarifa na unataka kuingia, kurekebisha, au kufuta taarifa zako za kibinafsi, unaweza kupata taarifa za mawasiliano kwenye ukurasa wa Mawasiliano ya Kulinda Taarifa.

Unapotutumia maombi yako, baada ya kutuma ushahidi kamili wa utambulisho wako na taarifa za kutosha zinazoturuhusu kutambua taarifa zako za kibinafsi, wanaohusika katika kudhibiti taarifa watazingatia ombi lako huku wakipima faida za mtu kuweza kuingia kwenye taarifa zake au kuzirekebisha au kufuta taarifa zake na masilahi ya tengenezo, kutia ndani labda ikiwa kukubaliwa kwa maombi hayo kunaweza kuhatarisha haki ya uhuru wa ibada na shughuli za tengenezo. Pia, tutampa taarifa mtu yeyote wa tatu kuhusu mabadiliko yanayohitajika.

Tafadhali zingatia kwamba huenda taarifa zako zisiweze kufutwa ikiwa sheria inataka zishughulikiwe au ikiwa zinahitaji kutunzwa kwa misingi mingine ya kisheria. Kwa mfano, shirika hili la kidini linaweka taarifa za kudumu za mtu zinazoonyesha kwamba yeye ni Shahidi wa Yehova. Kufuta taarifa ya aina hiyo kutaingilia utendaji wa tengenezo na imani ya dini. Maombi ya kufuta taarifa za kibinafsi yanategemea kutumwa kwa ripoti iliyotolewa mahakamani au hati inayoonyesha matakwa ya muda wa kutumia taarifa hizo. Pia, unaweza kupeleka malalamiko yako kwa wenye mamlaka ya kulinda taarifa kuhusu kutumiwa kwa taarifa ulizotupatia kupitia tovuti hii.