Hamia kwenye habari

MEI 15, 2023
RWANDA

Mvua Kubwa Zasababisha Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Magharibi mwa Rwanda

Mvua Kubwa Zasababisha Mafuriko na Maporomoko ya Ardhi Magharibi mwa Rwanda

Mei 2 na 3, 2023, mvua kubwa zilisababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi Magharibi mwa Rwanda. Zaidi ya watu 130 wamekufa na maelfu wamelazimika kuhama makao yao kwa sababu ya mvua. Mafuriko na maporomoko hayo ya ardhi, yameharibu mimea, nyumba, madaraja, na barabara.

Athari Ambazo Ndugu na Dada Zetu Wamepata

  • Hakuna ndugu au dada aliyejeruhiwa au kufa

  • Nyumba 51 zimeharibiwa kabisa

  • Nyumba 43 zimepata uharibifu mkubwa

  • Majumba 2 ya Ufalme yamepata uharibifu mdogo

Jitihada za Kutoa Msaada

  • Halmashauri 3 za Kutoa Msaada ziliteuliwa ili kusimamia jitihada za kutoa msaada unaohitajika

  • Washiriki wa Halmashauri ya Tawi na waangalizi wa mzunguko wanashirikiana na wazee wa makutaniko yaliyoathiriwa ili kuandaa msaada wa kiroho

Tunasali kwamba Yehova aendelee kuwategemeza ndugu na dada zetu nchini Rwanda wanaopitia “nyakati za taabu.”​—Zaburi 46:1.