Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 71

Sisi Ni Jeshi la Yehova!

Sisi Ni Jeshi la Yehova!

(Waefeso 6:11-14)

  1. 1. Sisi ni jeshi lake,

    Yehova Mungu,

    Ambalo latangaza,

    Ufalme wa Mungu.

    Yesu anatawala,

    Ndiye Mfalme.

    Tumejitolea

    Pasipo woga.

    (KORASI)

    Sisi ni jeshi lake,

    Yehova Mungu,

    Twatangaza kwamba

    “Anatawala.”

  2. 2. Sisi ni watumishi

    Wake Yehova.

    Twatafuta kondoo

    Wanaougua.

    Na chakula kuwapa

    Bila kuchoka;

    Tuwakaribishe

    Mikutanoni.

    (KORASI)

    Sisi ni jeshi lake,

    Yehova Mungu,

    Twatangaza kwamba

    “Anatawala.”

  3. 3. Jeshi lake Yehova

    Latii Kristo,

    Na tayari kwa vita,

    Likiwa imara.

    Laonyesha busara,

    Na ujasiri.

    Licha ya hatari,

    Liko imara.

    (KORASI)

    Sisi ni jeshi lake,

    Yehova Mungu,

    Twatangaza kwamba

    “Anatawala.”

(Ona pia Flp. 1:7; Flm. 2.)