Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 73

Tupe Ujasiri

Tupe Ujasiri

(Matendo 4:29)

  1. 1. Tutangazapo Ufalme,

    Na kukushuhudia.

    Kuna wapinzani wengi,

    Wanaotudhihaki.

    Hatutawaogopa,

    Kwa kuwa tunakutii.

    Tupe roho yako twaomba,

    Ee Yehova twakusihi.

    (KORASI)

    Tupe ujasiri Baba;

    Tushinde woga wetu.

    Tupe uhakika Baba,

    Tuzidi kuhubiri.

    Siku ya Har-Magedoni,

    Twajua iko karibu,

    Tupe ujasiri Baba.

    Twakuomba.

  2. 2. Japo twaweza kuhofu,

    Wajua umbo letu.

    Waahidi kutulinda,

    Na kututegemeza.

    Wanaotunyanyasa,

    Wazidipo kututisha,

    Tuwezeshe kusonga mbele,

    Kutangaza jina lako.

    (KORASI)

    Tupe ujasiri Baba;

    Tushinde woga wetu.

    Tupe uhakika Baba,

    Tuzidi kuhubiri.

    Siku ya Har-Magedoni,

    Twajua iko karibu,

    Tupe ujasiri Baba.

    Twakuomba.