Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 74

Shiriki Kuimba Wimbo wa Ufalme!

Shiriki Kuimba Wimbo wa Ufalme!

(Zaburi 98:1)

  1. 1. Wimbo huu, wa ushindi, wa shangwe;

    Wamtukuza Yehova Mungu.

    Na maneno yanahimiza watu,

    Imba nasi; wimbo wa Ufalme:

    (KORASI)

    ‘Abuduni Mungu nyote,

    Mwana Wake, Atawala.

    Jifunzeni wimbo mpya wa ’Falme.

    Yehova Mungu mmwinamie.’

  2. 2. Tunaimba, habari za Ufalme.

    Kristo Yesu; atawala juu.

    Taifa jipya lilitabiriwa,

    Kristo Yesu lamkaribisha:

    (KORASI)

    ‘Abuduni Mungu nyote,

    Mwana Wake, Atawala.

    Jifunzeni wimbo mpya wa ’Falme.

    Yehova Mungu mmwinamie.’

  3. 3. Wimbo huu ni rahisi kujua.

    Uko wazi; unachangamsha.

    Duniani, umati umejua,

    Nao pia waita wengine:

    (KORASI)

    ‘Abuduni Mungu nyote,

    Mwana Wake, Atawala.

    Jifunzeni wimbo mpya wa ’Falme.

    Yehova Mungu mmwinamie.’