Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

WIMBO NA. 87

Njooni! Mburudishwe

Njooni! Mburudishwe

(Waebrania 10:24, 25)

  1. 1. Leo ulimwengu umepotoka;

    Haumtambui Mungu.

    Mwongozo ufaao twahitaji,

    Peke yetu hatuwezi.

    Mikutano yetu huburudisha;

    Imani huimarisha.

    Inatuchochea kutenda mema,

    Inatufariji sana.

    Hatutaacha amri za Yehova;

    Wala kumtumikia.

    Twafunzwa mema kwenye mikutano;

    Ili tuipende kweli.

  2. 2. Mungu ajua mahitaji yetu;

    Neno lake tulitii.

    Tununue wakati wa kuwapo,

    Kwenye mikutano yote.

    Wanaume wamwogopao Mungu,

    hutufunza njia zake.

    Ndugu na dada zetu wa kiroho,

    Hututegemeza sana.

    Twatazamia wakati ujao,

    Kuona wapendwa wetu.

    Twafundishwa maisha yafaayo,

    Kwa hekima toka juu.