Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

JW LIBRARY

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Library (Windows)

Maswali Yanayoulizwa Mara Nyingi​—JW Library (Windows)

JW Library inategemezwa katika vifaa vinavyotumia mifumo ya uendeshaji ifuatayo:

  • Android 5.1 au mfumo wa karibuni zaidi

  • iOS 12.0 au mfumo wa karibuni zaidi

  • macOS iliyo na M1 au chip ya karibuni zaidi

  • Windows 10 toleo la 1903 au toleo la karibuni zaidi

Ili kuhakikisha kwamba JW Library ni salama na inategemeka, huenda pindi kwa pindi tukahitaji kuongeza matakwa ya msingi ya kutendesha programu hii. Kwa hiyo, tunapendekeza kwamba kila wakati uhakikishe unatumia mfumo wa uendeshaji wa karibuni zaidi kwenye kifaa chako. Ikiwa huwezi kusasisha kifaa chako kifikie matakwa ya msingi, huenda programu hiyo bado ikatumika, lakini hutaweza kutumia sehemu mpya za programu hiyo.

 

Lugha mpya huongezwa pindi kwa pindi. Ili uone orodha ya lugha ambazo chapisho unalotaka linapatikana, bonyeza kitufe cha Lugha.

Rangi hizo zinalingana na mpangilio wa vikundi vinane vinavyofafanuliwa kwenye Swali la 19 katika kijitabu Utangulizi wa Neno la Mungu.

 

JW Library inafanya kazi kwa njia ileile katika vifaa vyote. Lakini, sehemu fulani na matoleo mapya ya programu hutolewa wakati tofauti-tofauti kwa ajili ya matumizi katika kila kifaa.

 

Hapana. Ikiwa utaondoa programu ya JW Library na kuisakinisha tena upya, kumbukumbu ya alama za ukurasa na mistari uliyopiga itapotea. Lakini, ikiwa umefuta au kuondoa chapisho fulani na kisha ukalipakua tena, alama za ukurasa na sehemu ulizokuwa umepigia mistari zitapatikana tena.

 

Hapana. Kwa wakati huu, alama za kukumbuka ukurasa na sehemu ulizopigia mistari zitapatikana tu katika kifaa ulichofanya hivyo.

 

Tatizo: Baada ya kusasisha programu ya JW Library ili kupata toleo la hivi karibuni, huenda ukapata ujumbe unaosema kwamba mambo makuu uliyoandika na alama ulizoweka zimepotea. Huwezi kuona mambo makuu uliyoandika, vibandiko, alama, machapisho unayotumia kila mara na alama za kukumbuka kurasa.

Suluhisho: Toleo la hivi karibuni la programu hiyo inaweza kutatua tatizo hilo. Sakinisha toleo lenye nambari kubwa zaidi, na ufuate maelekezo yaliyo kwenye skrini ili kurudisha mambo yako makuu na alama.

 

Ikiwa unatatizika kupakua nakala zenye sauti au video, fuata hatua zifuatazo ili kuhakikisha kwamba maktaba za Video na Muziki zimewekwa vizuri katika Windows na kuchaguliwa katika JW Library.

  1. Fungua Folda, bofya tabo ya Mwonekano, kisha bofya menyu ya Kidirisha cha Uabiri halafu chagua Onyesha Maktaba.

  2. Katika kidirisha cha upande wa kushoto, tafuta na ufungue Maktaba.

  3. Utaona folda ya Muziki na folda ya Video. Ikiwa folda hizi hazipo, chagua Maktaba kwa kubonyeza upande wa kulia wa kipanya, kisha bofya Rejesha maktaba chaguo-msingi.

  4. Chagua folda ya Video na ubonyeze upande wa kulia wa kipanya, bofya Sifa, na utaona folda chini ya Mahali pa maktaba. Utahakikisha pahali penyewe baadaye katika vipimo kwenye JW Library. Kisha bofya Rejesha Chaguo-msingi.

  5. Chagua folda ya Muziki na ubonyeze upande wa kulia wa kipanya, bofya Sifa, na utaona folda chini ya Mahali pa maktaba. Utahakikisha pahali penyewe baadaye katika vipimo kwenye JW Library. Kisha bofya Rejesha Chaguo-msingi.

Mwishowe, fuata hatua zifuatazo ili kuhakikisha kwamba maktaba za Video na Muziki zimechagulia kwenye vipimo vyako vya JW Library:

  1. Fungua JW Library, kisha ubofye kitufe cha Vipimo.

  2. Kwenye Vipimo, hakikisha kwamba sehemu ya Hifadhi programu za sauti kwenye inahifadhi kwenye mahali pa maktaba pa Muziki na Hifadhi video kwenye inahifadhi kwenye mahali pa maktaba pa Video ambapo ulipata awali katika folda ya Kichunguzi Faili.

Ikiwa bado unapata shida kupakua faili za programu za sauti au video, hakikisha kwamba una ruhusa ya kuhifadhi faili kwenye folda ya Muziki na folda ya Video kwa kuweka faili mpya ndani ya kila folda. Ili kupata habari zaidi, ona sehemu ya usaidizi wa Microsoft au mwombe rafiki ambaye ana ujuzi wa kutumia Windows akusaidie.

 

Rafiki anayefahamu programu ya JW Library anaweza kukusaidia. Ikiwa hawezi, tafadhali wasiliana na ofisi ya tawi iliyo karibu.