Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Kitabu cha Yoshua

Sura

Muhtasari wa Yaliyomo

  • 1

    • Yehova amtia moyo Yoshua (1-9)

      • Soma Sheria kwa sauti ya chini (8)

    • Matayarisho ya kuvuka Yordani (10-18)

  • 2

    • Yoshua atuma wapelelezi wawili Yeriko (1-3)

    • Rahabu awaficha wapelelezi (4-7)

    • Rahabu apewa ahadi (8-21a)

      • Ishara ya kamba nyekundu (18)

    • Wapelelezi warudi kwa Yoshua (21b-24)

  • 3

    • Waisraeli wavuka Yordani (1-17)

  • 4

    • Mawe ya ukumbusho (1-24)

  • 5

    • Waisraeli watahiriwa kule Gilgali (1-9)

    • Sherehe ya Pasaka; mwisho wa mana (10-12)

    • Mkuu wa jeshi la Yehova (13-15)

  • 6

    • Kuta za Yeriko zaanguka (1-21)

    • Rahabu na familia yake waokolewa (22-27)

  • 7

    • Waisraeli washindwa kule Ai (1-5)

    • Sala ya Yoshua (6-9)

    • Dhambi yasababisha Waisraeli washindwe (10-15)

    • Akani afichuliwa na kupigwa mawe (16-26)

  • 8

    • Yoshua avamia Ai (1-13)

    • Jiji la Ai latekwa (14-29)

    • Sheria yasomwa kwenye Mlima Ebali (30-35)

  • 9

    • Wagibeoni wajanja watafuta amani (1-15)

    • Hila ya Wagibeoni yagunduliwa (16-21)

    • Wagibeoni watakuwa watekaji wa maji na wakusanyaji wa kuni (22-27)

  • 10

    • Waisraeli wawatetea Wagibeoni (1-7)

    • Yehova awapigania Waisraeli (8-15)

      • Mawe yawaangukia maadui wanaokimbia (11)

      • Jua lasimama tuli (12-14)

    • Wafalme watano wa maadui wauawa (16-28)

    • Majiji ya kusini yatekwa (29-43)

  • 11

    • Majiji ya kaskazini yatekwa (1-15)

    • Muhtasari wa ushindi wa Yoshua (16-23)

  • 12

    • Wafalme wa mashariki mwa Yordani washindwa (1-6)

    • Wafalme wa magharibi mwa Yordani washindwa (7-24)

  • 13

    • Maeneo ambayo hayajatekwa (1-7)

    • Kugawanywa kwa maeneo mashariki mwa Yordani (8-14)

    • Urithi wa kabila la Rubeni (15-23)

    • Urithi wa kabila la Gadi (24-28)

    • Urithi wa kabila la Manase upande wa mashariki (29-32)

    • Yehova ni urithi wa Walawi (33)

  • 14

    • Kugawanywa kwa maeneo magharibi mwa Yordani (1-5)

    • Kalebu arithi Hebroni (6-15)

  • 15

    • Urithi wa kabila la Yuda (1-12)

    • Binti ya Kalebu apewa eneo (13-19)

    • Majiji ya Yuda (20-63)

  • 16

    • Urithi wa wazao wa Yosefu (1-4)

    • Urithi wa kabila la Efraimu (5-10)

  • 17

    • Urithi wa kabila la Manase upande wa magharibi (1-13)

    • Maeneo zaidi kwa ajili ya wazao wa Yosefu (14-18)

  • 18

    • Maeneo yaliyobaki yagawanywa huko Shilo (1-10)

    • Urithi wa kabila la Benjamini (11-28)

  • 19

    • Urithi wa kabila la Simeoni (1-9)

    • Urithi wa kabila la Zabuloni (10-16)

    • Urithi wa kabila la Isakari (17-23)

    • Urithi wa kabila la Asheri (24-31)

    • Urithi wa kabila la Naftali (32-39)

    • Urithi wa kabila la Dani (40-48)

    • Urithi wa Yoshua (49-51)

  • 20

    • Majiji ya makimbilio (1-9)

  • 21

    • Majiji ya Walawi (1-42)

      • Ya wazao wa Haruni (9-19)

      • Ya Wakohathi waliobaki (20-26)

      • Ya Wagershoni (27-33)

      • Ya Wamerari (34-40)

    • Ahadi za Yehova zatimia (43-45)

  • 22

    • Makabila ya mashariki yarudi nyumbani (1-8)

    • Madhabahu yajengwa karibu na Yordani (9-12)

    • Kusudi la madhabahu laelezwa (13-29)

    • Mgogoro wasuluhishwa (30-34)

  • 23

    • Maneno ya mwisho ya Yoshua kwa viongozi wa Waisraeli (1-16)

      • Hakuna ahadi yoyote ya Yehova iliyokosa kutimia (14)

  • 24

    • Yoshua awakumbusha Waisraeli historia yao (1-13)

    • Awahimiza wamtumikie Yehova (14-24)

      • “Mimi na familia yangu, tutamtumikia Yehova” (15)

    • Yoshua afanya agano na Waisraeli (25-28)

    • Yoshua afa na kuzikwa (29-31)

    • Mifupa ya Yosefu yazikwa Shekemu (32)

    • Eleazari afa na kuzikwa (33)